Familia moja katika eneo la Kapkonga ,kaunti ndogo ya Keiyo kaskazini kaunti ya Elgeyo Marakwet wanakadiria hasara baada ya nyumba yao kuteketea mapema jumatano.
Akithibitisha mkasa huo,kamanda wa polisi katika eneo hilo ,Peter Mulinge alisema alipata ripoti kutoka kwa naibu chifu eneo hilo Laban Cherop kuwa nyumba ya Nicholas Rono mwenye umri wa miaka 80 imeteketea.
Kamanda huyo aidha alidokeza kuwa,inashukiwa kuwa moto huo ulisababishwa na hitilafu ya umeme akisema kuwa tayari uchunguzi umeanzishwa kubaini chanzo cha moto huo.
Hata hivyo,Mulinge alisema kuwa hakuna chochote kilichookolewa na hakuna mtu aliyeachwa na majeraha kutokana na kisa hicho.