Ziara ya Baraza la maaskofu wa kanisa katoliki mjini Roma Italia imeingia siku ya tatu hii leo.
Katika ziara hiyo,maaskofu hao wamehiji kaburi la mtakatifu Paulo na Petero ambaye ni mwanzilishi wa kanisa.
Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nyeri Anthony Muheria akizungumza katika kanisa la Mtakatifu Petero alisema kwamba lengo la ziara yao kuu mwaka huu ni kuhakikisha kwamba wanaimarisha uhusiano wao na mwenyezi mungu kando na shughuli zao za kawaida kupalilia shamba la bwana.
Aidha,askofu mkuu aliwashauri wakenya kuendelea kuungana mikono kuliombea taifa ili amani izidi kudumu na kwa manufaa ya mshikamano na uwiano wa taifa.