Serikali imeanza kuchunguza kampuni 16 jijini Eldoret zinazoaminika kuwalaghai wananchi pesa zao kwa lengo la kuwatafutia kazi ughaibuni.
Kwa mujibu wa katibu katika wizara ya Leba Shadrack Madime anasema kwamba,wamezitambua kampuni hizo ambazo anasema hazijapewa leseni za kuwapeleka wakenya ughaibuni hii ikitokana na ushirikiano wa wizara hiyo na idara ya Upelelezi DCI na washirika wengine.
Uchunguzi huo unafuatia taarifa kwa vyombo vya habari ambapo zaidi ya wakaazi jijini Eldoret mia tatu walilaghaiwa mamilioni ya pesa wakitumai kupata kazi Canada.
Hata hivyo,Mwadime amewataka wakenya kutuma maombi ya kazi kupitia taarifa inayotolewa na mamlaka ya kitaifa ya uajiri ,na zilizoidhinishwa mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo.
Vilevile,katibu huyo akiwataka wakenya wanaotafuta kazi nje ya nchi kuhakikisha inasajiliwa na wizara ya Leba kabla ya kutafuta stakabadhi zozote za usafiri ili kurahisishia kazi idara hiyo na kukomesha ulaghai.