Karama rohoni

Askofu wa jimbo katoliki la Ngong’  John  Obala Owaa amepongeza juhudi zilizopigwa na ujio wa kikindi cha wanakarama almaarufu Charistmatic Renewal akisema kwamba watu wengi duniani wamemtambua kristu na kuishi maisha yanayopendeza.

Akiongea wakati wa maadhimisho ya miaka hamsini tangu kubuniwa kwa kikundi cha wanakarama katika Kathedrali ya Mt.Yosefu Mfanyikazi Ngong’ askofu Owaa alisema kwamba neno lake kristu limeweza kusambaa kwa umbali kutokana na hatua hiyo,ambao msukumo wake ni maombi.

Hata hivyo,askofu Owaa aliwatahadharisha sana wakristu kutotumia roho  visivyostahili akidokeza kwamba wengi wa wakristu wamejiingiza kwa maswala yasiyofaa kutokana na kile wanaamini wanaongozwa na roho wake kristu.

Aidha,askofu huyo amewataka wakristu kila muda kumtanguliza roho mtakatifu ili maisha yao ya ukristu uweze kuimarika,akisema kwamba ni kupitia hiyo roho ndipo mkristu anaweza akawa karibu hata zaidi na mwenyezi mungu.

Ikumbukwe kuwa kikundi cha wanakarama  kilibuniwa Februari 1967 katika chuo kikuu cha Duauesne cha Pittsburgh Pennsylvania ,wakati profesa wa historia William Bill Storey alipobatizwa katika Roho Mtakatifu katika kikundi cha maombi cha Karismatiki Episcopal,utume wa huduma hiyo ikiwa na sehemu tatu ikiwa ni pamoja na Ubatizo katika Roho Mtakatifu,Umoja kati ya Wakristu na huduma kwa maskini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *