Mababa roma

Maaskofu wa majimbo mbalimbali nchini wanatarajiwa kuelekea Roma katika mkutano wa kawaida wa Kila baada ya miaka mitano.

Maaskofu hao wanatarajiwa kuwa Roma kuanzia jumatatu ya tarehe ishirini na sita Agosti.

Katika safari hiyo almaarufu ad limina ambalo ni Jina la kilatin, maaskofu wanatarajiwa kuhiji makaburi ya Mtakatifu Peter na Paulo mkutano wa pili ni kukutana ana kwa ana na Baba mtakatifu na kueleza Zaidi kuhusu jimbo kama njia moja ya  kusimika uhusiano kati ya jimbo na makao makuu ya kanisa takatifu katoliki lililo na makao yake mjini Vatican.

La tatu itakuwa ni ripoti ya Kila askofu kuhusu jimbo lake na haswa katika hatua na mikakati ya kiimani katika jimbo lake kama njia moja ya kueleza safari ya Imani katika majimbo mbalimbali nchini.

Ikumbukwe kuwa ziara hii iliidhinishwa mnamo tarehe 31st mwezi wa December 1909 na baba mtakatifu Pius.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *