Mwakilishi wa kike katika kaunti ya Elgeyo Marakwet Caroline Ngelechei amewadhahatarisha wanafunzi ambao wako likizoni dhidi ya utumizi wa dawa za kulevya na unywaji wa pombe.
Akiongea na kituo hiki mwakilishi huyo aliwataka wazazi katika kaunti hiyo kufuatilia kwa undani masomo ya wanao shuleni pamoja na mienendo yao wanapokuwa likizoni akidokeza kuwa wengi wa wazazi hawaipi kipao mbele masomo ya wanao na hata wale wanaotangamana nao.
Hata hivyo ngelechei aliwaomba wazazi kuwapa wanao mahitaji msingi shule zikitarajiwa kufunguliwa kwa muhula watatu juma lijalo ili kundeleza masomo yao.
Haya yanajiri huku visa vingi vya ukosefu wa nidhamu na ukiukaji wa maadili vikishuhudiwa miongozni wa kwa wanafunzi wengi humu nchini.