Acheni maovu

Ipo haja ya kumshukuru mwenyezi Mungu katika Kila jambo kwa kuwa shukrani ndio ufunguo wa karama za Mungu.

Padre mkuu wa eneo la kipastorali la Nandi Japheth Machichim akiongoza Misa ya shukrani kwenye shule ya wavulana ya Mtakatifu Mikaeli Terige,ametoa wito kwa Kila mmoja kujifunza kumshukuru mwenyezi Mungu katika Kila jambo kwa kuwa shukrani hizo huja na Amana kutoka kwake Mungu.

Alitoa wito kwa wanafunzi kuwa watiifu  siku zote kwa kuwa utiifu huo hubadilisha mambo magumu kuwa rahisi na kadhalika kuwapa mwelekeo wa maisha.

Alitoa wito kwa Kila mmoja kudhihirisha Imani Yao kwa matendo akisema kuwa Imani dhabiti itachangia ufanisi katika maisha ya kika binadamu.

Padre Machichim alitoa wito kwa wakristu kujiepusha na matendo maovu akisema kuwa mambo maovu ambayo yamejaa ndani ya nafsi huleta madhara makubwa maishani na badala yake watekeleze Imani ya kweli kwa kuonyesha matendo mema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *