Wakazi wa eneo la Kimalel kaunti ya Baringo wametoa makataa ya wiki mbili kwa serikali ya kaunti hiyo kuimarisha hali ya hospitali ya umma ya Kimalel la sivyo wataifunga.
Haya yanajiri baada ya huduma katika hospitali hiyo kuzorota kutokana na ukosefu wa vifaa muhimu.
Kulingana na wakaazi wa eneo hilo ni kuwa hospitali hiyo imesalia mahame kwa muda wa mwaka moja sasa, ambapo wagonjwa kutoka katika vijiji vya Koriema, Patakwen na Bekibon, wakilazimika kutafuta huduma za matibabu katika maeneo mengine kutokana na ukosefu wa maji na stima.
Hata hivyo gavana wa kaunti hiyo Benjamin Cheboi amesema kuwa anafahamu hali ya hospitali hiyo akihaidi kutafuta ufadhili ili kuboresha huduma katika hospitali hiyo.