Gavana wa uasin Gishu Jonathan Bii Chelilim ametangaza kuwa atamteua naibu gavana mpya kufuatia kujiuzulu kwa Mhandisi John Barorot.
Akizungumza hapa jijini Eldoret gavana Bii amesema kuwa atalituma jina la naibu gavana mteule, kwa bunge la kaunti hiyo ili kuhakikiwa na wawakilishi wadi, gavana Bii kadhalika anatarajiwa kutangaza mabadiliko zaidi katika uongozi wa serikali ya kaunti ya Uasin Gishu.
Bii aidha ameusifu ushirikiano kati yake na John Barorot tangu alipoingia afisini September mwaka wa 2022.
Awali Barorot alipuuzilia mbali madai kuwa kujiuzulu kwake kunatokana na kudorora kwa uhusiano kati yake na gavana Bii.
Wakaazi wa kaunti ya Uasin gishu nao wametoa hisia zao wakisema kuwa kuna mambo mengi ambayo huenda yakachochea Barorot Kujiuzulu wakidai kuwa gavana Bii hakufuata ushauri wa raia akichagua mgombea mwenza kuelekea uchaguzi wa mwaka wa 2022.