Aux.Lelei:Acheni maovu

Wakristu wametakiwa kujitenga na maswala ambayo yanaweza yawaka kizingiti kwa wao kuingia katika ufalme wa mbingu.

Akihubiri kwenye ibada ya mazishi katika eneo la Chepsaina kaunti ya Uasin Gishu,askofu msaidizi wa Jimbo katoliki la Eldoret John Lelei amesikitikia kile anasema wanadamu kujiingiza kwa mambo ambayo hayampendezi mwenyezi mungu akiwataka kuwa makini na hatua zozote wanazopiga maishani mwao.

Askofu lelei alisema kwamba mara mingi wakristu wanataka kuishi maisha yasiyokuwa na kujitolea akiwataka kuwa makini wasije wakaingia mitego ya wahubiri wa uongo au hata waganga.

Aliwataka wakristu kila mara kuwa waamnifu kwa kristu akitaja kwamba atawaongoza na kuwasaidia kustahimili majaribu na changamoto za maisha.

Aidha,askofu msaidizi huyo alitumia fursa hiyo kuwashauri wazazi kuhakikisha wanawapeleka wanao shuleni ndipo wawajengee maisha bora za siku za baadae.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *