Serikali imesema kuwa zaidi ya wanafunzi elfu mia moja na kumi na nane wametumiwa barua yakujiunga na vyuo mbalimbali nchini kupitia mfumo mpya wa kidijitali wa KUCCPS.
Kulingana na waziri wa elimu Profesa Julius Ogamba wanafunzi 118,000 tayari wamepokea barua zao kati ya maombi 125,000 yaliyotumwa.
Kauli hii ikitiliwa mkazo na rais William Ruto ambaye amewataka wazazi kulipa asilimia kumi ya karo ikizingatiwa kuwa serikali imekwisha gharamia asilimia tisini.