Msongo wa mawazo kero kubwa

Walimu wakuu wa shule zinazimilikiwa na kanisa katoliki nchini wanaendelea na warsha katika ukumbi wa chuo kikuu cha katoliki huku swala magonjwa ya kiakili uwajibikaji na malezi bora yakipewa kipaumbele.

Askofu msaidizi wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Simon Peter Kamomoe alitoa wito kwa walimu wakuu kuipa kipaumbele namna ya kukabiliana na msongo wa mawazo ambao hupelekea magonjwa ya kiakili akitoawito kwa walimu siku zote kuwa karibu na wanafunzi kama njia moja ya kuwapa motisha.

Naye askofu wa jimbo katoliki la Bungoma Mark Kadima alisema kuwa athari za utanndawazi ni miongoni mwa maswala tata katika malezi ambayo yanastahili kuangaziwa na walimu pamoja na wazazi kikamilifu.

Alitoa wito kwa waalimu kadhalika kupalilia nia zilizo njema ambazo zimenogeshwa katika imani ya kanisa katoliki akitoa wito kwa walimu wakuu wa shule hizo kuwa mfano bora na kuhudumia shule hizo kwa uadilifu.

Askofu Kadima alitoa wito kwa walimu hao wakuu kukabiliana kwa ukamilifu swala la utovu wa nidhamu katika shule mbalimbali akitoa wito kwa walimu hao kuhakikisha kuwa shule hizo zinasalia salamu dhidi ya nyanyaso mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *