Maziwa ya mama kinga mwilini

Huku wiki ya Unyonyeshaji ukiwa unaendelea kuadhimishwa kote duniani,kina mama nchini wameshauriwa kuwanyonyesha wanao kwa muda wa miezi sita bila kuwapa chochote kuwasaidia kupata kinga dhabiti mwilini.

Kwa mujibu wa mtaalamu  na mshauri wa lishe katika kaunti ya Elgeyo-Marakwet Pricillah Ng’etich ambaye amesikitia kile anasema kina mama wengi kukosa kuwanyonyesha watoto wao kwa muda mwafaka akisema inahatarisha maisha ya wanao.

Vilevile,mshauri huyo aliwataka kina mama kukumbatia lishe bora ili wanao waweze kuwa na afya bora na kuweza kukua vyema na kuimarika kwa akili zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *