Walaghai wajitoza kanisani

Kaimu Inspekta Jenerali wa polisi Gilbert Masengele amesema maafisa wa usalama wameanzisha uchunguzi kubaini kisa cha ulaghai wa mamilioni ya pesa kwa baadhi ya wakaazi katika kaunti ya Uasin Gishu.

Kulingana naye maafisa tayari wameanza uchunguzi wake kuhusu sakata ya sarafu mjini Eldoret ambapo wakaazi pamoja na viongozi wa dini walilaghaiwa.

Askofu wa kanisa la Dominion Eldoret Caleb Mwanya,anasema mshukiwa wa sakata hiyo Ambrose Makech aliyewalagahi alikua mmoja wa washiriki wa kanisa lake pamoja na familia yake na hakuna muda walimshuku kuwa ni mtapeli.

Hapo awali,gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jonathan Bii Chelilim aliwahakikishia wenyeji katika kaunti usalama wao na kuwajibishwa kwa watapeli watakaopatikana na hatia ya kuwapora wakaazi mali yao kupitia njia ya udanganyifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *