Hatutafanya kazi

Wafanyikazi wa chuo kikuu cha Moi Eldoret wameendelea kuandamana kulalamikia kile wanasema kukosa kukulipwa mishahara yao na usimamizi wa shule hiyo.

Wameomba idara ya Fedha kutoa pesa zitakazotumika kuwalipa huku wakilalamika kwamba mishahara yao imekua ikichelewa.

Wakati huo,wafanyikazi hao wametaka idara ya Fedha kubuni sera na mbinu mwafaka zitakazofanikisha malipo yao kwa njia inayostahili bila kushuhudiwa kwa mvutano unaowakabili kwa sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *