OLE SAPIT;Dumisheni amani mkiandamana

Askofu mkuu wa kiangilikana nchini Jackson Ole Sapit ametaka uwajibikaji miongoni mwa wakenya kutoka tabaka zote akisema swala la amani,utangamano na uwiano  unastahili kulindwa.

Akizungumza katika ibada iliyoandaliwa na kanisa la kianglikana huko Nyahururu kaunti ya Laikipia,askofu Ole Sapit amesisitiza wakenya kuwa waangalifu na chochote kile wanatekeleza akirejelea maandamano ya kupinga mswada wa fedha akiwataka waandamanaji kuandamana kwa amani bila kuharibu mali ya umma.

Vilevile,askofu huyo aliwataka maafisa wa usalama kukoma kutumia nguvu kupitia kiasi wanapowakabili waandamanaji akieleza ni haki yao kikatiba kuandamana kwa amani.

Askofu Ole sapit aidha,aliitaka serikali kusikiliza kilio cha wakenya akisema maelewano baina yao itatatua maswala yanayo isibu taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *