mpeni kaisari yaliyo yake

Seneta wa kaunti ya Uasin Gishu Jackson Mandago amewataka magavana nchini kuhakikisha wanawalipa wanakadarasi kwa muda mwafaka kwa lengo la kufanikisha maendeleo.

Mandago alisema miradi nyingi ya Maendeleo zimekwama kutokana na wanakandarasi waliotwikwa jukumu hizo kukosa kulipwa na serikali za kaunti kwa wakati mwafaka.

Akitoa mfano wa kaunti ya Isiolo ambayo anasema kuna uhaba wa makafani,senata huyo amesema swala hilo limewafanya wakaazi kaunti hiyo kutafuta huduma hizo kwenye  kaunti jirani kama Embu na Meru ,swala hili akisema linachangiwa na kutolipwa kwa wanakandarasi hao.

Aidha,seneta huyo aliwashauri magavana kutenga fedha za kutosha kwenye miradi ya maendeleo ambazo zimesalia miaka nenda miaka rudi ili kutimiza matakwa ya wapiga kura.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *