Mbingu ni kwa weupe kama pamba

Askofu wa jimbo katoliki la Meru Saleius Mugambi amewataka wakristu kuimarisha imani yao kwa kristu ili waweze kuutwa ufalme wa mbingu.

Akihubiri katika kanisa la Christ the King Marimanti,askofu Mugambi alisema, ni wajibu wa kila mmoja kujiweka tayari kuwa mfuasi wake kristu na pia kuwasaidia wengine kupokea huo mwaliko wake mwenyezi mungu.

Aliwataka wakristu kuwa kilelezo chema kwa wale ambao hawajamtamua kristu kwa kuyatenda ambayo yanaambatana na mafundisho yake mwenyezi mungu.

Askofu Mugambi aidha,aliwataka wakritu kusaidia kanisa kwa miradi mbalimbali ya maendeleo iwe ni ujenzi wa hekalu au maswala mengine ya kimsingi ya kusaidia uenezaji wa injili inadumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *