Selemundu inaweza dhibitiwa

Ulimwengu ukiadhimisha siku ya ugonjwa wa selemundu,wito umetolewa kwa wazazi na wakenya kutambua kuwa ugonjwa huo unaweza kudhibitiwa kwa kuzingatia maagizo ya wataalam.

Akizungumza katika hospitali ya Rufaa ya Moi Eldoret,mtaalam wa ugonjwa selemundu kwenye hospitali hiyo Dkt.Festus Njuguna alisema kwamba watu wengi hawana ufahamu wa ugonjwa huo,akiwataka kuhakikisha wanatembelea hospitali wanapotambua dalili zozote kwa wanao.

Vilevile,daktari huyo alisema kwamba ugonjwa wa Selemundu husababishwa na chembechembe za mwili au genes kutoka kwa wazazi na usambazwa kutoka kizazi hadi kizazi na tiba yake ni kufanyiwa upasuaji wa mishipa za damu maarufu bone marrow transplant.

Aidha,alisema kwamba kila mwaka wanawapokea zaidi ya watoto mia nane wanaotambuliwa kuwa na ugonjwa wa Selemundu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *