Msongo wa mawazo ni Real

Kuna haja ya jamii kuwa mstari wa mbele kuwasaidia vijana na kila mmoja anayepambana na msongo wa mawazo kimawaidha ili waweze kujitoa kwenye hali hiyo na kuendelea na shughuli zao za kawaida.

Kwa mujibu wa askofu msaidizi wa jimbo katoliki la Eldoret John Kiplimo Lelei,visa vingi vya maafa miongoni mwa vijana huchangiwa na jamii kuwapuuza waathiriwa na swala hilo lisipotatuliwa mapema,huenda kizazi cha kesho kikakosa mwelekeo.

Alisisitiza haja ya jamii kuungana mikono kukabiliana na unyanyapaa ambao mara si moja umechangia watu kujitoa uhai. Aidha,amewataka waathiriwa kuhakikisha wanatafuta ushauri kutoka kwa vikundi mbalimbali ambavyo wanahisi huenda vikawasaidia kimawaidha na suluhu la kudumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *