Maporomoko tumeyazika

Serikali ya kaunti ya Nandi imesema inalenga kukabili maporomoko yanayoshuhudiwa kila mara katika eneo bunge la Tindiret kwa kuimarisha ukuzaji na uzalishaji wa mmea wa kahawa.

Akiongea katika eneo la Lengon wadi ya Kapchorua ,gavana wa kaunti ya Nandi Stephen Sang alisema kwamba kwa muda mwingi wenyeji eneo hilo wamekumbana na janga hilo na watahakikisha ukulima wa kahawa unaimarika kusaidia kukabiliana na maporomoko hayo.

Alisema sharti ardhi iliyoharibiwa kutokana na ukataji miti ovyo kukabiliwa na kuwasaidia wakulima kupata mapato ya kujikimu nayo.

Ikumbukwe kuwa zaidi ya wakaazi 500 waliathirika na maporomoka hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *