Bishop Lelei; siku ya kwanza afisini

Askofu msaidizi wa jimbo katoliki la Eldoret John Kiplimo Lelei ameanza kazi rasmi hii leo baada ya kupata daraja la Askofu huku akihaidi kutekeleza mambo mengi jimboni kwa ushirikiano na Askofu wa jimbo katoliki Dominic Kimengich.

Askofu John Kiplimo Lelei ndiye Askofu msaidizi wa pili katika jimbo katoliki la Eldoret tangu jimbo kubuniwa daraja ambalo anasema kuwa limekuja na majukumu mengi tofauti na kama alivyokuwa padre mkuu wa jimbo katoliki la Eldoret.

Amehaidi kufanya kazi pamoja na makanisa mbalimbali ili kueneza injili na kuongoza jamii ya Mungu katika njia inayofaa licha ya tofauti ya kiimani, akisema kuwa viongozi wote wa kidini sharti washirikiane kama njia moja ya kuongoza taifa la Mungu katika ramani ya mbinguni.

gIkumbukwe kuwa Askofu john Kiplimo Lelei aliteuliwa na Baba mtakatifu Francisko tarehe ishirini na saba mwezi wa tatu mwaka huu kuwa msaidizi wa jimbo katoliki la Eldoret.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *