KCCB:Serikali isiweke nta sikio

Baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini limekariri msimamo wao wa hapo awali kuwa mswada wa kifedha wa mwaka 2024 unanuia kumkandamiza mkenya mlipa ushuru.

Baraza hilo likiongozwa mwenyekiti wake ambaye pia ni askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Kisumu Maurice Muahatia Makumba lilikariri msimamo wao wa kupinga baadhi ya mapendekezo ya matozo katika mswada huo ambao anasema kuwa huenda ikamsakama mkenya mlipa ushuru.

Askofu mkuu Muhatia alishabikia juhudi za vijana almaarufu Gen Z ambao wamejitokeza wa kutaka mageuzi katika mswada huo akisema kuwa juhudi zao zinaonyesha ujasiri na uzalendo ambao utapiga jeki demokrasia nchini.

Alitoa wito kwa serikali kutotia gundi sikioni kuhusu maswala hayo ya vijana akitoa wito kwa polisi kadhalika kutumia hekima ili kusiwepo na majeruhi na maafa.

Askofu mkuu aliwakanya vijana hao dhidi ya kutumiwa na watu walio na nia fiche akisema kuwa huenda kukawa na wale walio na lengo la kuvuruga amani nchini kwa sababu ambazo hazieleweki.

Alisema kuwa kanisa katoliki halipingi ulipaji wa ushuru nchini bali kile kanisa linataka liangaziwe zaidi na kuwepo na kiasi fukani katika kuwatoza wakenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *