Askofu wa jimbo katoliki la Machakos Norman King’oo Wambua amenyoshea kidole cha lawama serikali ya kitaifa kwa kufinyilia chini hospitali za kibinafsi nchini.
Askofu King’oo alisema hatua ya bima ya kitaifa NHIF kukosa kuwalipa wahudumu wa afya wa nyanjani imelemaza shughuli za utoaji huduma kwenye hospitali hizo za kibianfsi.
Akiongea katika eneo la Matungulu ,kaunti ya Machakos Askofu King’oo hospitali za kibinafsi ziko kwenye hatari ya kufungwa kwa kushindwa kuwalipa wahudumu wa afya na hata usambazaji duni wa madawa.
Aidha,aliitaka serikali kuhakikisha inatatua swala la kufanyiwa mageuzi bima mpya ya afya ili kuziba mihanya zilizopo kwa sasa na kusaidia hospitali za kibinafsi kuendelea na shughuli zake kwa njia mwafaka.