Haki idumumishwe

Askofu msaidizi wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Wallace Nga’nga amewataka wakristu kuwa wale wanaosimamia haki kila wakati.

Akihubiri wakati wa hafla za Family Day ya Thika Deanary,askofu Nga’nga amesema ukristu unasisitiza uwepo wa uwazi na kuwajali wengine bila kuegemea tofauti zao za kimaisha.

Askofu Nga’nga alisema wengi wa watu katika jamii ambao ni wanyonge wameteseka kwa kunyanyaswa na kukosa kupata haki kwa kuwa hakuna anayesimama nao dhidi ya wanaowakosea akiwataka wakristu kuomba kristu aweze kuwaongoza kila muda kwa kutenda hak.

Aidha,askofu huyo msaidizi alisisitiza haja ya wakristu kuishi maisha ambayo yanaweza kuigwa na wengine katika jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *