Haiti ipo nchini

Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich ameitaka serikali ya kitaifa kusitisha azma yake ya kuwatuma maafisa wa usalama kwenda nchi ya Haiti na badala yake kuhakikisha kwamba amani inarejeshwa kwenye maeneo mbalimbali nchini yanayoshuhudia utovu wa usalama nchini.

Akizungumza katika eneo la Kinyach mpakani mwa kaunti za Elgeyo-Marakwet na Baringo wakati alipoongoza misa ya amani,askofu Kimengich ametaka serikali kutilia maanani usalama wa wananchi wake kabla ya hatua zozote za kuwapeleka maafisa wake nje ya nchi.

Aidha,askofu Kimengich alisisitiza haja ya wakenya kushirikiana katika jamii kupambana  na utovu wa usalama na aina yoyote ya uhalifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *