Afisa mkuu mtendaji mpya wa Hospitali ya mafunzo na Rufaa ya Moi Eldoret Dkt.Philip Kirwa amebaini kuwa kuanzia juni mwaka huu mfumo mpya wa kutumia bima ya afya ya SHIF itaanza kutumika rasmi kwenye hospitali hiyo.
Akizungumza baada ya kuwasili kwa jukumu la kusimamia MTRH,Kirwa amesema kuwa kurejeshwa kwa bima hiyo ya afya itachangia pakubwa kupunguza msongamano na mrundiko wa faili za wagonjwa walioshinda kulipia ada za matibabu kwa afya bora ya jamii.
Dkt.Kirwa amewashauri wakenya kutopuuza mwito wa kujipatia bima hiyo akiwaeleza kwamba itawafaidi kwa kupunguza gharama ya matibabu.
Aidha,afisa huyo amepongeza mipango ya kuainisha shughuli za matibabu kwenye hospitali hiyo kwa kuruhusu hospitali mbalimbali za umma kutoa huduma sawia ya hospitali hiyo kwa hili akisema kuwa,itasaidia kupunguza foleni ndefu na hata wagonjwa wengine kukosa kuhudumiwa.
Amewashauri wafanyikazi katika hospitali hiyo kuhakikisha wanashirikiana vyema ili kuwahudumia umma pasi na ugumu wowote.