Acheni manunguniko

Wito umetolewa kwa wakristu kuhakikisha kwamba wanajitenga na manunguniko kila wakati katika maisha yao ila wawe wale wa kushukuru na kidogo walichopewa.

Kwa mujibu wa askofu mteule wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Monsinyo Simon Peter Kamomoe ni kwamba kila mwanadamu ametengewa kile kilicho chake na yawapaswa kuwa wanatoa shukrani kwani mwenyezi mungu huwabariki kwa uwezo wa kila mmoja.

Askofu huyo mteule alisikitishwa na kile anasema wakristu wamesahau mafundisho ya kuwa na moyo wa kutosheka na kile kidogo wamebarikiwa nacho akiswashauri kurejelea mafudisho ndipo waweze kuyapanua mawazo yao.

Aidha,monsinyo Kamomoe alisisitiza haja ya kuwepo kwa ujirani mwema msimu wa krwaesma unapoendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *