wakulima ukanda wa North Rift wanapitia mchujo husiokua na mwisho kutokana na foleni ndefu kwenye maghala ya kitaifa bewa la Eldoret bila ya mbolea msimu wa upanzi ukiwa unawadia.
Wakizungumza katika makao makuu ya maghala ya kitaifa na mazao ya NCPB Eldoret,wakulima hao wamesikitikia kile wanasema muda wao mwingi kuharibika na hawapati mbolea yenye ruzuku.
Walisisitiza haja ya serikali ya kitaifa kuhakikisha inaweka mikakati na sera za kutosha kuhakikisha wakulima wote wanapata mbolea hiyo kwa muda mwafaka.
kadhalika,walionyesha hofu ya kuchelewa mwaka huu kupanda mimea yao kutokana na safari zao za kupanda na kushuka kwenye magahala hayo.