Wenyeji katika kaunti ya Uasin Gishu walieleza kuridhishwa na ujio wa kifaa cha redio ambacho wanasema imewaunganisha wao na watu kutoka tabaka mbalimbali na maeneo mbalimbali.
Wakiongea mjini Eldoret,wenyeji hao walisema redio imekua mojawapo ya vifaa ambavyo vinawakutanisha watu waliopoteleana kando na ukaribu wake kwa watu hata walio mashinani.
Aidha,wakaazi hao waliwapongeza wanahabari kwa kufanikisha shughuli za kufikisha ujumbe kwa umma unatimia tena kwa wakati unaofaa.
Siku hiyo ilitangazwa na nchi wanachama wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO mnamo mwaka 2011. Kisha siku hiyo iliidhinishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo Januari 14, 2013 kuwa siku ya kimataifa.
Kenya kwa sasa ina zaidi ya vituo 100 vya redio, na idadi ya vituo vinavyomilikiwa na watu binafsi na mashirika inaendelea kuongezeka.
Licha ya changamoto hizo, wengi wanakisia kuwa redio itastahimili mawingi ya changamoto zinazosababishwa na mabadiliko ya kasi ya teknolojia na kuendelea kuwa chombo cha kutegemewa cha mawasiliano katika kuwataarifu, kuwaelimisha na kuwaburudisha wasikilizaji wake.