Gavana wa kaunti ya Elgeiyo Marakwet Wesley Rotich amewahimiza wakaazi wa kaunti hiyo kukumbatia upanzi wa mimea na ufugaji kama njia moja ya kurejesha amani na kujipatia riziki.
Akizungumza katika shule ya wasichana ya Metkei gavana huyo amesema kuwa tayari serikali yake imeleta mimea mbalimbali kwa wakaazi wa kaunti hiyo, akitoa wito kwa wakaazi haswa wale wanaoishi katika maeneo ya mipaka kukukumbatia upanzi na ufugaji kama njia moja ya kuhakikisha kuwa kila mkaazi amepata angalau mradi utakaompa riziki ya kila siku.
Gavana huyo kadhalika ametishia kuwachukulia hatua ya kuwaweka korokoroni Yule ambaye atazembea katika zoezi hilo la upanzi.