KIU YA MASOMO

Shule za upili nchini zinaendelea kuwapokea wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza kufuatia agizo la serikali la mpito wa asilimia mia moja ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane (KCPE) kujiunga na kidato cha kwanza.

Katika mahojiano ya kipekee na idhaa hii afisini mwake, mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Central hapa mjini Eldoret Shadrack Makumu, ameelezea kuridhishwa kwake na idadi ya wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza katika shule hiyo.

Alisema kufikia sasa jumla ya wanafunzi 95 wamejiunga na kidato cha kwanza wakitarajia idadi hiyo kuongezeka hadi 101 kulingana na nafasi zilizosalia.

Aidha, aliwaomba wazazi kuwaelekeza vyema watoto wao ili kuepukana na marafiki wabaya ambao watawapotosha kimaadili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *