Wakaazi wa kaunti ya Uasin Gishu wametakiwa kuishi na kutangamana pamoja kama njia moja ya kufanikisha mshikamano wa kaunti ya Uasin Gishu.
Haya ni kwa mujibu wa mbunge wa Kapseret Oscar Sudi ambaye amewataka wakaazi wa kaunti kuendelea na biashara yao bila woga akitoa wito kwa wakaazi hao kamwe kutokubali kutenganishwa kwa misingi ya kikabila.
Kuhusu kupanda kwa gharama ya maisha nchini Sudi ametoa wito kwa wakenya kuvumilia hali ilivyo kwa sasa akisema kuwa tayari rais Willian Ruto ameweka mikakati kabambe ya kufufua uchumi wa taifa hili akihoji kuwa taifa litafurahia matunda hayo hivi karibuni.