Wakristu wametakiwa siku zote kuiga mfano wa Elizabeti kwa kuvumilia yale wanayoyapitia na kusali daima kwa kuwa Mungu hutimiza ahadi yake kila wakati.
Askofu wa jimbo katoliki la Nakuru Cleophas Oseso Tuka akihubiri katika misa ya kusherehekea miaka ishirini na tano ya mtawa Agnes Njeri eneo la Gilgil jimbo katoliki la Nakuru askofu Oseso ametoa wito kwa kila mkristu kudumu siku zote katika sala pasi na kukoma kwa kuwa Mungu ndiye mtimiza ahadi
Ametoa wito kwa wakristu kadhalika kujifunza kumshukuru Mungu katika kila jambo kwa kuwa shukrani hiyo huja na baraka ya kipekee kwa maisha ya binadamu.