Kina mama msingi bora

Wito umetolewa kwa kina mama kuwa mstari wa mbele kuwaelekeza wana wao kwa njia ya kiimani na kuwajengea msingi bora wana hao.

Akihubiri katika eneo la Momoi Lower Subukia,askofu wa jimbo katoliki la Nakuru Cleophas  Oseso Tuka amesema kina mama wana nafasi nzuri nay a karibu kwa watoto tangu kuzaliwa kwao na iwapo watawaelekeza vyema jamii itawapata watu wenye nidhamu na viongozi wa kutegemewa siku za usoni.

Aliwataka kuwa mfano mwema kwa matendo yao mema na kujisadaka bila ya kujibakisha katika kutafuta uso wake mwenyezi mungu.

Wakati huo askofu Tuka aliwasihi wakristu kumruhusu mwenyezi mungu awaongoze maishani mwao kwa kujiepusha na mambo ambayo yatawasongesha mbali na mwenyezi mungu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *