Bishop Kimengich; Fuateni amri ya Mungu

Wakristu wameshauriwa kuimarisha imani yao kwa kristu kwa kuzishika na kuzifuata na sheria zake huyo kristu.

Akihubiri katika kanisa la Moyo Mtakatifu wa Yesu Kathedrali,askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic KImengich amesema kwamba sheria zilizopo za kristu ndizo mwongozo bora kwa mkristu anayelenga kujikatia tiketi ya kuingia mbinguni, akiwataka wasimame imara kiimani.

Askofu Kimengich Vilevile amewataka wakristu kuomba mwongozo wa sheria hizo ili waweze kuwa na moyo wa kukata kauli kwa njia ya haki bila ya mapendeleo yoyote.

Aidha,askofu Kimengich amewataka watoto kuheshimu wakubwa wao maana ni sheria ambayo inawasaidia kuitwa wana wa mungu na kujitenga na vikundi visivyokuwa na msingi wowote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *