Askofu wa jimbo katoliki la Eldoret Dominic Kimengich amemtaka kila mmoja katika jamii kumwelekeza mtoto ambaye anasema ni kioo cha jamii.
Akizungumza afisini mwake mjini Eldoret,askofu Kimengich amesema kwamba mtoto anapokwenda kinyume na maadili ni jamii nzima ndio itatumbukia kwenye mauti na inapasa kila mmoja kujukumika kimaadili ili kurejesha maadili mema katika jamii.
Vilevile,askofu Kimengich amesisitiza haja ya wenyeji kuwa makini msimu huu wa mvua nyingi ya Elnino kwa kuwaweka watoto karibu wasiwe waathirwa wa mafuriko na pia kwa wao kumanikania mwito wa kujiepusha na maeneo hatari zilizotajwa na idara ya utabiri wa hali ya hewa.
Askofu Kimengich alitumia fursa hiyo kuwahimiza wakristu kutilia maanani kwamba wanapaswa kushiriki ibada za kila wakati wa kuabudu ndipo wasije wakajisahau kwa shamrashamra za sherehe na kumtenga kristu.