Mjitume kimaisha

Serikali ya kaunti ya Uasin Gishu imesisitiza kwamba inafanya kila liwezalo kuhakikisha kwamba ukosefu wa ajira kwa maelfu ya vijana inashughulikiwa kuwapa nafasin kujituma kupitia ubunifu wao wenyewe.

Akizungumza na kituo hiki,waziri wa barabara,uchukuzi na miundomsingi kaunti hii Mhandisi Joseph Lagat amesema kwamba kuna maeneo ya vifutio ambavyo vijana wanaweza wakawekeza kwa kupanda aina tofauti ya mimea na maua huku akisema soko iko tayari kwa bidhaa zao.

Lagat vilevile alisema kwamba ili kukabiliana na hali ngumu ya maisha wakaazi wanastahili kuungana mikono kwa ushauri wa kusonegsha mbele uchumi wa taifa akiwaeleza kwamba wajitolee kufanya kazi bila ya kuchagua kazi hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *