Afya kwa wote

Serikali imeweka mikakati ya kufanikisha sheria mpya ya afya iliyopitishwa hivi majuzi katika bunge la kitaifa.

Akizungumza mjini Eldoret katibu katika wizara ya afya Mary Muthoni amewataka wakenya kukumbatia sheria hiyo mpya ya UHC akisema itawafaa wakenya wa tabaka zote kwenye hospitali mbalimbali nchini.

Aliwataka wakenya kukoma kuingiza siasa katika maswala yanayohusu afya na badala yake kuungana na serikali ili kufanikisha mpango huo nchini.

Katibu huyo alisema kuwa wizara hiyo imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa data za wakenya zinahifadhiwa kidijitali kama njia moja ka kurahisisha huduma na  kuepuka mirundiko ya fomu katika haspitali mbalimbali nchini

Alisema kwa serikali itaajiri  wahudumu wa afya nyanjani kama njia moja ya kupiga jeki huduma ya afya katika hospitali mbalimbali za humu nchini.  

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *