Muungano wa masorovea nchini umeelezea kughadhabishwa kwao na mabadiliko ya sheria za ardhi iliyopitishwa nchini ukisema kuwa mabadiliko hayo yatamkandamiza mkenya.
Wakizungumza mjini Eldoret muungano huo wa masorovea umetoa wito kwa wizara ya ardhi na serikali kusitisha mabadiliko hayo ys sheria za ardhi wanayonuia kuanza kutekeleza wakisema kuwa yatawanyima wakenya wa kawaida huduma za sajili za ardhi.
Masorovea hao kadhalika wemetaka wizara ya ardhi wamepinga mswada ambao umewasilishwa katika bunge la seneti unaohus mali isiyohamishika ya real estate act wa mwaka wa 2023 wakisema kuwa itamtwika mkenya wa kawaida mzigo zaidi.
Wamehoji kuwa pendekezo hilo linanuia kuipa serikali nguvu zaidi katika maswala hayo ya ardhi nah ii itakuwa na athari kubwa kwa wananchi