Askofu wa jimbo katoliki la Bungoma Mark Kadima ametoa wito kwa mapadri na watumishi wote wa kanisa kutochagua eneo ambalo wangependa kuhudumu.
Akihubiri wakati wa hafla ya daraja la Upadrisho katika jimbo katoliki la Bungoma, askofu Kadima amesema kwamba wakristu katika pembe zote za ulimwengu wana kiu ya kujengwa kiimani na iwapo watumishi katika shamba la bwana watachagua mahali wanakotumwa, itaathiri pakubwa ukuaji wa imani.
Wakati huo,askofu huyo amesisitiza haja ya makleri na majandokasisi kuwa na hulka ya kushirikiana na wengine ili neno la mwenyezi mungu liweze kuenezwa kote.