Kamba yanyonga Wakenya

Wakaazi wa hapa mjini Eldoret wameibua hisia zao kufuatia matamshi ya waziri wa Kawi Davis Chirchir ambaye anasema kuwa huenda bei ya petroli hapa nchini ikapanda hadi shilingi mia tatu kwa kila lita.

Waziri wa Kawi Davis Chirchir amenukuliwa akisema kuwa iwapo vita kati ya Hamas na Israel itaendelea basi mamlaka ya kawi nchini haitakuwa na budi ila kuongeza bei hiyo kutoka kwa hali ilivyo kwa sasa hadi shilingi mia tatu.

Wakaazi hao sasa wanatoa wito kwa serikali kutafuta mbinu mbadala ya kuwashughulikia mwananchi wa kawaida wakidai kuwa tangu serikali ya Kenya kwanza kuingia madarakani hali ya kiuchumu imekuwa ya juu…..

Sasa wametaka serikali kupunguza ushuri inayotoza wakenya wakisema kuwa hali ilivyo kwa sasa imewasakama mno.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *