Walinda usalama wamulikwa Transzoia

Idara ya usalama katika kaunti ya Transnzoia imetakiwa kuimarisha doria katika eneo la maili saba, ili kukabili utovu wa usalama unaoshuhudiwa katika eneo hilo.

Hii ni kufuatia kisa cha mtu mmoja kuuliwa kwa kudungwa kisu wengine wawili wakijeruhiwa vibaya siku chache zilizopita, huku wakaazi wakisema kuwa visa hivyo hutekelezwa na baadhi ya wakaazi wanaotambulika katika eneo hilo.

Mwakilishi wa eneo hilo Simon Murey amewaomba maafisa wa usalama katika eneo hilo, kuwajibikia changamoto hiyo kikamilifu kwani baadhi yao wanasemekana kuzembea kwenye majukumu yao wenyeji wakizidi kuhangaishwa na wahalifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *