upanzi wa mianzi

Shule ya upili ya wasichana ya Wiyeta katika kaunti ya Trans-Nzoia inayopakana na chemchemi ya Seiwa, imekumbatia uhifadhi wa mazingira na hasa ndege aina ya korongo kupitia upanzi wa miti aina ya mianzi (Bamboo).

Wanafunzi hao walichukua jukumu la kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa kuhifadhi chemchemi hiyo kupitia maonyesho ya kitaifa ya kilimo yanayofanyika mjini Kitale.

Aidha, mwalimu mkuu wa shule hiyo Esther Kibor alisema wamekuwa wakikuza miche ya mianzi ili kupiga juhudi za uhifadhi wa mazingira kadhalika kutumia mti huo katika kutengeneza bidhaa mbalimbali zikiwemo fanicha.


Aliongeza kuwa fedha zinazopatikana kupitia uuzaji wa bidhaa za bamboo hutumika kukuza talanta za wanafunzi shuleni humo.

Mmoja wa wanafunzi kutoka klabu ya mazingira shuleni humo ameelezea umuhimu wa mianzi katika kukabili athari za mabadiliko ya tabianchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *