Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Philip Anyolo Subira amewataka kuwa na subra badala ya kujiingiza kwenye ndoa ya mapema.
Akihubiri katika shule ya upili ya wasichana ya Huruma Jijini Nairobi,askofu mkuu alisema kwamba vijana wanastahili kukomaa kabla ya kuingia kwa ndoa kama njia moja ya kukabiliana na Changamoto zilizo kwenye wito huo.
Alitoa wito kwa watu wazima walio na uzoefu katika ndoa kuwakuza na kuwaelekeza vyema vijana hao ili kizazi kijacho kiwe na mwelekeo uliobora.