SIKU YA AFYA YA AKILI

Ulimwengu unaopadhimisha siku ya afya ya akili ,wito umetolewa kwa wakenya kuhakikisha kwamba wanaepukana na maswala ambayo huenda yakachangia kujipata waathiriwa wa ugonjwa wa kiakili.

Kwa mujibu mwanasikolojia katika hospitali ya Rufaa ya Moi Eldoret Dkt.Robina Momanyi ni kwamba yapo maswala mengi ambayo huchangia watu kuwa na ugonjwa wa kiakili ikiwemo msongo wa mawazo na kukosa kupata usaidizi.

Amesema yapasa wakaazi kupata hamasisho la kutosha kuhusiana na swala hili la afya ya akili.

Kadhalika,Dkt.Eunice Temet amesema kwamba kila mwaka hospitali ya rufaa ya Moi Eldoret MTRH inasajili wagonjwa wa akili 1000 kila mwaka akiwashauri walioathirika kutafuta huduma ndipo waweze kuwa salama dhidi ya ugonjwa huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *