SINODI;Kipaumbele ushirikishwaji

Askofu wa jimbo kuu katoliki la Nyeri Anthony Muheria ameelezea matumaini makubwa katika kongamano la Sinodi linaloendelea mjini Vatican.

Akiwa mmoja wa maaskofu wanaowakilisha baraza la maskofu wa kanisa katoliki nchini KCCB askofu Muheria alisema kuwa kongamano hilo limetoa fursa nzuri wa ushirikishwaji katika mambo tofauti, ukiwemo kusikiliza na kutoa mwongozo na kisha baadaye kutembea pamoja.

Alitoa wito kwa familia mbalimbali kadhalika kuwa na muda mwafaka wa kuipa kila muda wa kuongea na kusikizwa akisema kuwa hii ndiyo njia ya kipekee itakayounganisha na kuimarisha familia.

Ikumbukwe kwamba baraza la maaskofu wa katoliki nchini KCCB linawakilishwa askofu mkuu Anthony Muheria na mwenzakewa jimbo kuu la Mombasa Martin Kivuva Musonde ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *