Wazazi wametakiwa kumakinikia majukumu ya malezi kama njia moja ya kuboresha maadili miongoni mwa watoto wachanga nchini.
Haya ni kwa mujibu wa Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Askofu mkuu Philip Anyolo ambaye nasema kuwa watoto wengi nchini wamekosa kwa kiasi kikubwa malezi msingi kutoka kwa wazazi, akiwataka wazazi kujirudia na kuchukua nafasi yao ya malezi kikamilifu ili kukuza kizazi kijacho.
Askofu huyo amekariri kuwa malezi mazuri kutoka kwa wazazi ndio itakayowapa vijana maarifa ya kukabiliana na changamoto ambayo huenda ikawakodolea macho katika siku za usoni, akisema kuwa kule kuwatelekeza watoto wakiwa wachanga huenda ikaleta madhara makubwa zaidi ndani ya kizazi kijacho.