wakulima wataka serikali mahindi yao nchini inunuliwe

Wakulima wa mahindi katika kaunti ya Uasin gishu wametoa wito kwa serikali kumakininkia swala ya kununua zao hilo kwa wakulima wa hapa mchini badala ya kuagiza kutoka katika mataifa ya kigeni.

Wakiongozwa na mwenyekiti wa wakulima hao Kipkorir Menjo, wamesema kuwa wakulima wengi kwenye eneo hilo la bonde la ufa wangali wamesalia na  mahindi yao wakitaka serikali itilie maanani ununuzi wa mahindi hayo kutoka kwa wakulima wa humu nchini badala kununua kutoka mataifa ya kigeni akisema hatua hiyo itawazuia wakulima wengi nchini kukosa soko.

Kuhusu bei ya nafaka nchini wakulima hao wametoa wito kwa serikali kupandisha bei ya gunia moja ya kilo tisini kwa shilingi elfu tano ili wapate faida kutokanana gharama  ya juu ya  pembejeo  waliotumia  wakati wa upanzi kiptaigur Mias ni mkulima katika kaunti ya Uasin gishu.

Kadhalika wametoa wito kwa serikali kupitia wizara ya kilimo kuwaletea wakulimu vifaa vya kukausha mahindi wakisema kuwa mvua kubwa ambayo imeshuhudiwa majuma machache yaliyopita imeathiri miale ya jua jambo ambalo limesababisha kutoakauka kwa mahindi mengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *