Wito umetolewa kwa waristu kujieusha nakinyongo ,wivu na majivuno maana kila mwanadamu aliumba kwa njia moja ila wezo tofauti.
Akihubiri katika kanisa la St.Peter and Paul Cathedral wakati wa hafla ya Family Day jimbo katoliki la Embu,mwakilishi wa baba Mtakatifu nchini na Sudan Kusini Mwadhama Herbatus Matheus Maria Van Megen aliwataka wakristu kutambua kuwa kila mmoja ametunukiwa uwezo tofauti na kule kuonyesha majivuno huenda ikamtenga mja na muumba wake kwa kuwa Mungu anachukizwa na majivuno hayo.
Vilevile mwadhama Van Megen alisisitiza haja ya wakristu kutambua kwamba mwenyezi mungu anawatambua wote na ushirikiano wao kila mara inastahili kuwa jambo la msingi na la kutiliwa maanani kila mara wanapo tangamana.
Aidha,aliwataka wakristu kuwa watu wa haki katika maisha yao kila mara ndipo mwenyezi mungu aweze kuwatunuku na kuwabariki katika utendakazi wao.